1 Chronicles 2

Wana Wa Israeli


1 aHawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:
Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni,
2Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.

Yuda

Hadi Wana Wa Hesroni


3 bWana wa Yuda walikuwa:
Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni pa Bwana, kwa hiyo Bwana alimuua.
4 cTamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.


5 dWana wa Peresi walikuwa:
Hesroni na Hamuli.

6 eWana wa Zera walikuwa:
Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.

7 fMwana wa Karmi alikuwa:
Akari,
Akari maana yake Taabisha; pia anaitwa Akani ( Yos 6:1-26; 22:20 ).
ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.

8 Mwana wa Ethani alikuwa:
Azariya.

9 hWana wa Hesroni walikuwa:
Yerameeli, Ramu na Kalebu.

Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni


10 iRamu alimzaa
Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.
11Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi,
12 jBoazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.

13 kYese akawazaa
Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,
Au: Shima, maana yake Sifa njema (pia 1Sam 16:9; 17:13 ).

14wa nne Nethaneli, wa tano Radai, 15wa sita Osemu, na wa saba Daudi. 16 mDada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli. 17 nAbigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

Kalebu Mwana Wa Hesroni

18Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni. 19 oAzuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri. 20 pHuri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.
21 qHatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu. 22Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi.
23 r(Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.

24 sBaada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.

Yerameeli Mwana Wa Hesroni


25 Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:
Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.
26Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.

27 Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:
Maasi, Yamini na Ekeri.

28 Wana wa Onamu walikuwa:
Shamai na Yada.
Wana wa Shamai walikuwa:
Nadabu na Abishuri.
29Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.

30 Wana wa Nadabu walikuwa
Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.

31 Apaimu akamzaa:
Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani.
Sheshani akamzaa Alai.

32 Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:
Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.

33 Wana wa Yonathani walikuwa:
Pelethi na Zaza.
Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.

34 Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu.
Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha.
35Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.

36 tAtai akamzaa Nathani,
Nathani akamzaa Zabadi,

37 Zabadi akamzaa Eflali,
Eflali akamzaa Obedi,

38 Obedi akamzaa Yehu,
Yehu akamzaa Azaria,

39 Azaria akamzaa Helesi,
Helesi akamzaa Eleasa,

40 Eleasa akamzaa Sismai,
Sismai akamzaa Shalumu,

41 Shalumu akamzaa Yekamia,
naye Yekamia akamzaa Elishama.

Koo Za Kalebu


42 Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:
Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.

43 Hebroni alikuwa na wana wanne:
Kora, Tapua, Rekemu na Shema.
44Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai.
45 uShamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.
46Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.

47 Wana wa Yadai walikuwa:
Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.
48Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana. 49 vPia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa.
50 wHawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu.

Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa:
Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu,
51Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.

52 Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:
Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi,
53 xpamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.

54 yWazao wa Salma walikuwa:
Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori,
55 zpamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.
Copyright information for SwhKC